1. EBOLA NI NINI?
Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi
vijulikanavyo kitaalam (Ebola Virus). Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa
yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za virusi zinazosababisha kutoka damu
mwilini.
2. MTU ANAWEZAJE
KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA EBOLA?
Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa wa Ebola toka kwa mtu mwingine
aliyeambukizwa, au toka kwa wanyama kama nyani, ngedere, sokwe na popo.
Ugonjwa wa Ebola unaambukizwa kwa haraka kutoka mtu mmoja hadi
mwingine kupitia njia zifuatazo:-
• Kugusa majimaji ya mwili toka kwa mtu aliyeambukizwa virusi
vya Ebola - damu, matapishi, jasho, mkojo, mate, machozi, kamasi
• Kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa Ebola
• Kugusa godoro, shuka, blanketi, au nguo zilizotumiwa na
mgonjwa wa Ebola
• Kuchomwa na sindano au vifaa visivyo safi na salama
• Kugusa mizoga au kula wanyama pori kama vile Sokwe,nyani na
popo
• Kula matunda yaliyoliwa nusu na Wanyama


3. Nani wapo katika
hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa Ebola?
Kila mtu yupo katika hatari ya kuambukizwa na virusi vya Ebola, hata hivyo makundi ya
watu wafuatao wapo kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya Ebola:
• Watu wote wanaoishi na/
au kumhudumia mgonjwa wa Ebola
• Waombolezaji ambao
wanaweza kugusa mwili wa marehemu kama sehemu ya utaratibu wa mazishi
• Wawindaji wa msituni ambao wanaweza kugusa mizoga ya wanyama
• Watoa huduma za afya
4. Dalili za ugonjwa wa
Ebola ni zipi?
Dalili
za ugonjwa wa Ebola huanza kujitokeza kati ya siku 2 hadi 21 baada ya
kupata maambukizi. Mgonjwa wa Ebola huwa na dalili zifuatazo:
•
Homa kali ya ghafla
•
Maumivu ya kichwa
•
Maumivu ya mwili, misuli
na viungo
•
Kuharisha (kunakoweza
kuambatana na
•
damu)
•
Kutapika (kunakoweza
kuambatana na
•
damu)
•
Vipele mwilini
•
Kutokwa na damu puani,
mdomoni,
•
machoni, masikioni na
sehemu ya haja
•
ndogo na kubwa
•
Kuvia damu chini ya
ngozi
5. Wakati gani mtu
akapate matibabu?
Nenda
haraka kwenye kituo cha kutolea huduma za afya pindi unapohisi kuwa na
dalili za ugonjwa wa Ebola, au unapogusana na mtu mwenye dalili za
ugonjwa wa Ebola. Na pia, ni
muhimu kutoa taarifa haraka kwenye kituo cha kutolea huduma za afya
kilicho
karibu nawe pindi unapohisi mtu ana
dalili za ugonjwa wa Ebola.

6. Je, ugonjwa wa
Ebola unatibika?
Ugonjwa wa Ebola hauna tiba maalum wala chanjo. Mgonjwa
anashauriwa kuwahi kituo cha kutolea
huduma ya afya ili aweze kupatiwa tiba saidizi kulingana na dalili alizonazo
kama vile:
•
Tiba ya homa na maumivu
•
Kuongezewa maji mwilini
•
Tiba lishe
7.
Nifanye nini ili kujikinga na ugonjwa wa Ebola?
Njia za kujikinga na ugonjwa huu ni :-
•
Epuka kusalimiana kwa
kushikana mikono au kukumbatiana
•
Epuka kugusa damu,
matapishi, mkojo, kinyesi, kamasi, mate, machozi na maji maji mengine
yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa huu
•
Epuka kugusa au kuosha
maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola badala yake toa taarifa kwa
uongozi wa serikali ili wasimamie taratibu za mazishi
•
Epuka kutumia nguo,
shuka, blanketi, kitanda na godoro za mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu
• Nawa mikono kwa maji
yanayotiririka na sabuni mara unapomtembelea mgonjwa hospitalini au kumhudumia
nyumbani
•
Epuka kugusa wanyama
kama vile popo, nyani, sokwe, tumbili na swala au mizoga ya wanyama
•
Zingatia ushauri na
maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na viongozi wa serikali kuhusu
ugonjwa wa Ebola
•
Wahi kituo cha kutolea
huduma za afya uonapo dalili za ugonjwa wa Ebola
•
Toa taarifa mapema
kwenye kituo cha huduma za afya, ofsi ya serikali ya mtaa au kijiji uonapo mtu
mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola au kifo.
•
Zingatia usafi binafsi
pamoja na usafi wa mazingira yako.
-manyanda health
Comments