Mwanamke ambaye ana mazoea ya kula
vyakula vyenye mafuta mengi na sukari bila ya kutumia matunda kwa wingi,
yumo kwenye hatari ya kutopata uja uzito, utafiti unasema.
Utafiti
uliofanyiwa wanawake 5,598, uliwapata wale ambao wana mazoea ya kula
vyakula vyenye mafuta mengi, mara 4 au zaidi kwa wiki, wanachukua zaidi
ya mwezi mmoja kupata uja uzito, kuliko wanawake ambao hawatumii kabisa
chakula cha aina hiyo.
Walaji wengi wa chakula cha aina hiyo, pia
sio rahisi kupata mimba, katika kipindi cha mwaka mzima, hayo ni kwa
mujibu wa ripoti ya uzazi wa binadamu.
Wataalamu wanasema kwamba, lishe bora huboresha uwezekano wa kushika mimba.
Hata
hivyo, kumekuwa na changamoto fulani na utafiti huo, ukiwemo swala la
wanawake kujaribu kukumbuka, kile walichokuwa wa kila wakati wana uja
uzito.
Wanawake nchini Australia, New Zealand, Ireland na
Uingereza, waliulizwa kuhusiana na kile walichokuwa wakila mwezi mmoja
kabla ya kushika mimba, hasa wakati wa mimba yao ya kwanza.
Wakunga waliwatembelea kina mama hao, walipokuwa na mimba ya wiki 14
hadi 16, na wakaulizwa ni mara ngapi walikula matunda, mboga za majani
na samaki, mbali na chakula kama burgers, pizza, kuku wa kukaangwa
pamoja na vibanzi, kutoka katika migahawa inayouza vyakula vya mafuta
mengi na sukari.
Watafiti hao walibaini kuwa, wanawake wanaotumia
matunda mara tatu kwa mwezi, wanachukua kiwango cha nusu mwezi kwa
wastani kushika mimba, kuliko wale ambao wamekula matunda mara tatu au
zaidi kwa siku.
Pia walipiga hesabu kuwa, ''wanawake walio na
kiwango kidogo mno cha ulaji wa matunda mwilini, wako kwenye hatari ya
12% ya kutokuwa na uwezo wa kushika mimba katika kipindi cha chini ya
mwaka mmoja, huku hali kama hiyo ni asilimia 16% ya wale ambao wamekula
chakula kilicho na mafuta mengi, mara nne au zaidi kwa wiki.
Hii kwa ujumla ni hatari kwa asilimia 8% katika kundi sawa na hilo.''
Watu waliooana hawakutumika katika utafiti huu, hasa ikiwa mpenzi wa kiume alikuwa akipokea matibabu ya uzazi.
Mhadhiri
Claire Roberts, kutoka Chuo kikuu cha Adelaide, Australia, ambaye
aliongoza jopo la watafiti hao, anasema: "Matokeo hayo, yanaonyesha
kuwa, ulaji chakula bora, kinachojumuisha matunda na upungazaji wa
chakula chenye mafuta mengi na sukari, yatapunguza pakubwa muda wa
kushika mimba kwa wanawake."
Hata hivyo, huku watafiti hao
wakipata uhusiano uliopo kati ya utumiaji wa matunda na chakula chenye
mafuta mengi, kwa uwiano wa muda unaochukua mwanamke kutunga mimba,
lakini cha ajabu utafiti wao haukupata chochote dhidi ya uhusiano wa
ulaji maboga na samaki.
Daktari Gino Pecoraro, mhadhiri mkuu wa
Chuo Kikuu cha Queensland, ambaye hakujumuishwa katika utafiti huo,
anasema kuwa, "Kwa ujumla, utafiti huo, hauungi mkono, jinsi wataalamu
wa vyakula, wanavyoamini - wanaosema kuwa vyakula vyenye lishe bora, ni
vizuri kwa wanandoa kuwasaidia kupata mimba."
-bbc swahili
Comments