Vyakula vyenye wanga kwa wingi husababisha wanawake kukoma hedhi mapema, utafiti umeeleza.
Ulaji
wa tambi na wali kwa wingi kwa wanawake nchini Uingereza kunasababisha
kuwahi kukoma kwa hedhi mwaka mmoja na nusu mapema zaidi ya wastani wa
umri wa miaka 51.Hata hivyo, utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Leeds kwa wanawake 914 nchini Uingereza , pia umebaini kuwa mlo ulio na mafuta ya samaki kwa wingi na njegere na maharage unaweza kuchelewesha ukomo wa hedhi kwa wanawake.
Lakini wachambuzi wanasema kuna sababu nyingine, zikiwemo jenetiki
Haijafahamika ni kwa ukubwa gani ulaji chakula unaweza kuleta athari kwa wanawake kama tafiti zinavyoeleza.
Utafiti ulichapishwa kwenye jarida la Afya la Epidemiology & Community Health na wanawake waliulizwa mlo wao huwa una vyakula gani
Mlo wenye mboga za jamii ya kunde kwa wingi, kama vile njegere,maharage,maharage membamba na dengu kwa wastani huchelewesha ukomo wa hedhi
Vyakula vya wanga,hasa wali na tambi, vimeelezwa kusababisha ukomo wa hedhi mapema zaidi.
Sababu nyingine zilizoainishwa na watafiti ni pamoja na uzito wa mwanamke, Historia ya uzazi na waliopata tiba za homoni, lakini hawakuangalia sababu za kijenetiki
Janet Cade ni mtaalam wa lishe, anasema umri ambao ukomo wa hedhi huanza unaweza ''kuleta madhara makubwa'' kwa baadhi ya wanawake.
Wanawake ambao hedhi zao hukoma mapema wako kwenye hatari ya kupata maradhi ya moyo na maradhi ya mifupa, na wanaochelewa wanaweza kupata maradhi ya saratani ya matiti,tumbo na Ovari
![]() |
Vyakula jamii ya kunde vinaelezwa kuchelewesha ukomo wa hedhi kwa wanawake |
source: bbc
Comments