LEO tutaelezea kwa kina chanzo cha magonjwa ya moyo ambayo husumbua watu wengi. Chanzo kikubwa ni watu kutozingatia kanuni za ulaji bora, ni moja ya mambo yanayoongeza uwezekano wa mtu kupata magonjwa ya moyo. Kwa mfano, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, vyakula vyenye sukari nyingi, chumvi nyingi na lehemu nyingi , huku ulaji wa mbogamboga na matunda ukiwa ni wa kiwango cha chini, huongeza uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo. Lakini pia hali ya kuwa na uzito uliozidi kiasi au kuwa na unene uliopitiliza pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo mara kwa mara, huchochea uwezekano wa mtu kukumbwa na magonjwa ya moyo. Wakati mwingine magonjwa ya moyo huweza kutokana na historia ya ugonjwa huo katika familia. Umri unapozidi miaka 50 kuna uwezekano pia wa kupatwa na magonjwa haya ya moyo, huku wanaume wakiwa kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili mapema zaidi ikilinganishwa na wanawake. Magonjwa ya moyo huanza kumwandama mtu pale mambo fulani ...
1. EBOLA NI NINI? Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kitaalam (Ebola Virus). Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za virusi zinazosababisha kutoka damu mwilini. "Ugonjwa huu unaathiri binadamu na wanyama kama vile nyani, ngedere, sokwe na popo." 2. MTU ANAWEZAJE KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA EBOLA? Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa wa Ebola toka kwa mtu mwingine aliyeambukizwa, au toka kwa wanyama kama nyani, ngedere, sokwe na popo. Ugonjwa wa Ebola unaambukizwa kwa haraka kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia njia zifuatazo:- • Kugusa majimaji ya mwili toka kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola - damu, matapishi, jasho, mkojo, mate, machozi, kamasi • Kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa Ebola • Kugusa godoro, shuka, blanketi, au nguo zilizotumiwa na mgonjwa wa Ebola • Kuchomwa na sindano au vifaa visivyo safi na salama • Kugusa mizoga au kula wanyama pori kama vile Sok...